Friday, May 11, 2018

WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA WANUFAIKA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO


Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (wapili kushoto) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na wakazi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Vijana wajasiriamali waosha magari wa Kikundi cha  Msingi Mikwanja Car Wash yenye thamani ya shilingi milioni 1 iliyotoka katika fedha ya mfuko wa jimbo la Ukonga.Ni mwendelezo wa kutimiza ahadi ambazo Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara aliziahidi kwa wakazi wa jimbo hilo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),John Mrema.

Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto) akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Guruka Kwalala uliopo katika kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika mtaa huo leo kwa ajili ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza ahadi za Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko,Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto,Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala,   Dorcas Rukiko, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo wakikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash, Ally Mfaume (Wapili kulia) na Katibu Wake,Yasini Omary jijini Dar es Salaam leo.Uongozi wa Kata na mtaa pamoja Viongozi kutoka Chadema wamekabidhi mashine mbili za kuosha magari kwa Vikundi  vya Vijana wajasiamali waosha magari wa Mtaa wa Guruka Kwalala.

Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (kushoto) akizungumza jijini Dar es Slaam leo na Vijana wa Kikundi kingine cha Vijana wajasiriamali kitwaacho Nyamachoma kinachofanya kazi ya kuosha magari maeneo ya Gongo la  mboto Mwisho wa lami katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni 1 iliyotoka katika fedha ya Mfuko wa jimbo la Ukonga ikiwa  ni Mwendelezo wa kutimiza ahadi alizoahidi Mbunge wa Jimbo hilo,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyamachoma Car Wash,Juma Sungamizi,Katibu wa kikundi,Jimmy Vitalis na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema.

    Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi(watatu kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Mashine ya Kuosha magari iliyokabidhiwa leo kwa Kikundi cha Nyamachoma Car wash kilichopo Gongo la Mboto mwisho wa lami jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo na Vijana wajasiriamali wa Kikundi cha Kuosha magari kiitwacho Nyamachoma Car Wash katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa kikundi hicho yenye thamani ya shilingi Milioni 1 kutoka katika Mfuko wa Jimbo la Ukonga.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Katibu wa Kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari kiiitwacho Nyamachoma Car Wash,Jimmy Vitalis (wapili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho,Juma Sungamizi jijini Dar es Salaam leo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akipeana mikono ya pongezi na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukabidhi mashine mbili za kuosha magari na pikipiki kwa Vikundi viwili vya waosha magari Nyamachoma Car Wash na Msingi Mkwanja Car Wash vilivyopo katika Mtaa wa Gruruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo.

Wednesday, March 21, 2018

NGORONGORO HeROES YAIPIGA MSUMBIJI MABAO 2-1

 Kocha wa timu ya Vijana ya Msumbiji, Vicror Matine, akitoa maelekezezo kwa wachezaji wake hawapo pichani katika mchezo dhidi ya Tanzania


 Wachezaji wa timu ya Ngorongoro Heroes wakishingilia baada ya kupata bao la pili didi ya Msumbiji

Mashabiki wa mpira wakiishangilia timu ya Taifa ya Tanzania Ngorongoro Heroes wakati ilipokuwa ikichez na timu ya vijana ya Msumbiji

Wednesday, March 14, 2018

SERENGETI BOYS WAENDELEA NA MAZOEZI UWANJA WA KARUME DAR ES SALAAM. PICHA NA DOUBLE J BLOG

 Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam. PICHA NA DOUBLE J BLOG

Mkurugenzi wa benchi la ufundi wa timu za vijana, Kim Paulsen (akiwaelekeza wachezajiwa timu ya Serengeti Boys wakati walipokuwa wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Karume Dar es Salaa. PICHA DOUBLE J BLOG

Sunday, March 4, 2018

KILIMANJARO MARATHON YAFANA WAKENYA BADO WATESA WACHUKUA MEDARI ZOTE KM 42


Mshindi wa kwanza mbio Km: 42 Kilmanjaro Marathon, Cosmas Muteti, kutoka nchini Kenya, akimaliza mbio zake wakati wa michuano ya hiyo iliyofanyika  Moshi mkoani Kilimanjaro jana iliyodhaminiwa na Bia ya Kiliomanjaro. 


Waziri wa Habarai Utamaduni Sanaa na Michezo. Dk, Harison Mwakyembe, kushoto, akimvisha medali mshindi wa pili wa mbio za Tigo Kilimanjaro Marathon Km 21, Failuna Abdi, Mtanzania wakati wa michuano hiyo iliyofanyika Mosho mkoani Kilimanjaro


Mshiriki wa mbio za Tigo Kilimanjaro Marathon Km 21, Joram Mollel maalufu babu: katikati, akimaliza mbio wakati wa mashindana hayo yaliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.

 Mshindi wa Kwanza Km 42 wanawak, Flavious Kwamboka, akimaliza mbio za Kilimanjro Marathon zilizofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro


 Wanariadha wakijianda kukimbia

 Mwanariadha akiwa amechoka

 Wanariadha wa Tigo Kilimanjaro Marathon Km 21

 Wanariadha wa Kenya Km 42 wakichuana vikali katika mashindano hayo

  Wanariadha wakipokea maji

Mwanaridha wa km 21 akikimbia katika mbio za Kilimanjaro Marathon yalioofanyika mkoani Kilimanjaro March 4 /2018

Wednesday, February 28, 2018

Thursday, February 22, 2018

MEYA WA JIJI LA DAR ES SAAM, ISSA MWITA, KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA MEYA WA MJI WA BLANTYRE NCHINI MALAWI, WILD NDIPO, JIJINI DAR ES SALAAM


Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kushoto), akisalimiana na mgeni wake Meya wa Jiji la Blantyre, Wild Ndipo, walipokutana akiwa na ujumbe wa madiwani watatu ofisini kwakwe na kufanya mazungumzo.
PICHA DOUBL J BLOG

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto akizungumza na ujumbe wa wageni kutoka Nchini Malawi, Meya wa jiji la Blantyre Wild Ndipo katikati na madiwani wake walipomtembelea leo ofisini kwakwe. PICHA DOUBL J BLOG