Mkurugenzi wa Taasisi
ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna
Haule akitoa elimu ya vicoba endelevu kwa wanachama wa Kikundi cha
Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12
ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alialikwa kuwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Mwalimu wa Wateule
Vicoba, Glory Munisi akitoa elimu kuhusu elimu ya fedha wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho kilichopo Ulongoni jijini Dar es Salaam
jana. Wateule Vicoba inajumla ya vikundi 7
chini ya ,Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Fahari Tuamke Maendeleo, Neema Mchau akizungumza wanachama wa Kikundi cha
Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni kuhusu masuala ya kuthamini familia
pamoja na kuimarisa ndoa wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi
hicho jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wanachama
wa Wateule Vicoba wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa katika maadhimisho
hayo.

No comments:
Post a Comment