Saturday, November 23, 2019

TAASISI YA UWEZESHAJI WAJASIAMALI YA OPEN MIND AND THOUGHTS ORGANIZATION (OMTO) YALETA NEEMA KWA WATANZANIA

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia), Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakionyesha kwa pamoja Mkoba wa nyaraka za Taasisi ya OMTO katika uzinduzi wa taasisi hiyo . yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kulia) akizungumza na wajasiriamali pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola.

Mwakilishi wa Ofisi ya serikali ya mtaa ya Kitunda, Mwanahawa Zinga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) iliyochini ya Vicoba endelevu uliofanyika ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.  Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola akizungumza na wajasiriamali pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana. Vicoba Endelevu ni mwamvuli wa taasisi ya OMTO.



Baadhi ya Wanachama wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) pamoja na vikundi vingine vilivyopo chini ya Vicoba endelevu wakisikiliza kwa makini mada zinazoendelea wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.







       Baadhi ya wageni Waalikwa wakizungumza katika hafla hiyo.



Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (wa pili kushoto) akiitambulisha Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto), Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule, Mkurugenzi wa taasisi ya Data Sustainable Development Organization (Data), Sihaba Madenge na Mkurugenzi wa Taasisi ya Women Movement and Effort Organization (Wmeo), Anna Basita wakitumbuiza wakati wa hafla  ya uzinduzi wa taasisi OMTO yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watoto wa wanachama wa OMTO wakitumbuiza wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Taasisis ya OMTO uliofanyika ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto) akimlisha keki Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kushoto) akikabidhi keki kuashiria shukrani kwa Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola.

Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akikata utepe katika uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule.

Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akizungumza katika hafla hiyo.


Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) imesajiliwa rasmi tarehe 5/8/2019 ikiwa na ruhusa ya kufanya kazi ndani ya Tanzania na bara kwa kuzingatia lengo kuu la serikali la kuboresha maisha kwa kila mtanzania.

Taasisi hii imeona umuhimu wa kusaidiana na serikali na kuhakikisha lengo kuu la serikali kuwa na Tanzania ya viwanda linatimia.

Akizungumza Mkurugenzi wa OMTO, Anna Haule " Taasisi hii ina malengo yafuatayo kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kijamii, kushawishi jamii kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali, kuhasisha jamii kuwa na tabia ya kuweka akiba ili kukuza mitaji na kufanya biashara endelevu pamoja na kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiamali". Alisema Mkurugenzi.

Taasisi kwa sasa inavikundi 15 kwa hapa Dar es Salaam na mikoni yenye jumla ya wanachama 600 ikiwemo wanawake ni 85% na wanaume ni 15%.

Kwa elimu wanayoipata ya kuweka akiba na kufanya ujasiamali wa pamoja baadhi ya vikundi tayari wameshaanza kufanya ujasiriamalikwa utengenezaji wa batiki, sabuni za maji na pilipili ya embe malengo ni kuanzisha kilimo (green house), ufugaji wa kuku, samaki na nyuki.

Nae Raisi wa Vicoba Endelevu, Mhe. Devotha Likokola akizungumza "Miongoni mwa fursa zilizopo ni kuwa pamoja katika kufanya ujasiamali ili kuwekeza kutimiza malengo ya nchi yetu ya Tanzania ya viwanda na imani kubwa ni kufikia kuwa na viwanda vidogo vidogo na kwa baadae kuwa na viwanda vikubwa". Alisema Raisi.

                  HABARI PICHA KATIKA MATUKIO




















No comments:

Post a Comment