Friday, May 11, 2018

WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA WANUFAIKA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO


Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (wapili kushoto) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na wakazi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Vijana wajasiriamali waosha magari wa Kikundi cha  Msingi Mikwanja Car Wash yenye thamani ya shilingi milioni 1 iliyotoka katika fedha ya mfuko wa jimbo la Ukonga.Ni mwendelezo wa kutimiza ahadi ambazo Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara aliziahidi kwa wakazi wa jimbo hilo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),John Mrema.

Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto) akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Guruka Kwalala uliopo katika kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika mtaa huo leo kwa ajili ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza ahadi za Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko,Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto,Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala,   Dorcas Rukiko, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo wakikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash, Ally Mfaume (Wapili kulia) na Katibu Wake,Yasini Omary jijini Dar es Salaam leo.Uongozi wa Kata na mtaa pamoja Viongozi kutoka Chadema wamekabidhi mashine mbili za kuosha magari kwa Vikundi  vya Vijana wajasiamali waosha magari wa Mtaa wa Guruka Kwalala.

Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (kushoto) akizungumza jijini Dar es Slaam leo na Vijana wa Kikundi kingine cha Vijana wajasiriamali kitwaacho Nyamachoma kinachofanya kazi ya kuosha magari maeneo ya Gongo la  mboto Mwisho wa lami katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni 1 iliyotoka katika fedha ya Mfuko wa jimbo la Ukonga ikiwa  ni Mwendelezo wa kutimiza ahadi alizoahidi Mbunge wa Jimbo hilo,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyamachoma Car Wash,Juma Sungamizi,Katibu wa kikundi,Jimmy Vitalis na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema.

    Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi(watatu kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Mashine ya Kuosha magari iliyokabidhiwa leo kwa Kikundi cha Nyamachoma Car wash kilichopo Gongo la Mboto mwisho wa lami jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo na Vijana wajasiriamali wa Kikundi cha Kuosha magari kiitwacho Nyamachoma Car Wash katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa kikundi hicho yenye thamani ya shilingi Milioni 1 kutoka katika Mfuko wa Jimbo la Ukonga.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Katibu wa Kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari kiiitwacho Nyamachoma Car Wash,Jimmy Vitalis (wapili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho,Juma Sungamizi jijini Dar es Salaam leo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akipeana mikono ya pongezi na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukabidhi mashine mbili za kuosha magari na pikipiki kwa Vikundi viwili vya waosha magari Nyamachoma Car Wash na Msingi Mkwanja Car Wash vilivyopo katika Mtaa wa Gruruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo.