Saturday, May 22, 2021

WATOTO WA KITUNDA WAFAIDIKA NA TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION

 Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe akizungumza na wazazi pamoja na watoto wa kata ya Kitunda katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo katika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo. Taasisi hiyo yenye kauli mbiu ya '' Malezi ya watoto na michezo vinaanzia katika jamii '' imetoa jezi za michezo katika mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda ikiwa ni miongoni mwa kusapoti sekta ya michezo nchini.   
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe (Kushoto), Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Lutgarda Mbuya, Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike na Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile wakikabidhi jezi kwa mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo lililofanyika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike akizungumza katika hafla hiyo.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Lutgarda Mbuya akizungumza na wazazi na watoto wa kata ya Kitunda wakati wa Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo katika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Sauti ya Jamii wa kata ya Kitunda, Claudia Gabriel, akizungumza katika hafla hiyo.

Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile akizungumza na wazazi pamoja na watoto wa kata ya Kitunda jijini Dar es Salaam leo katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids  and Youth Foundation.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe, Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Lutgarda Mbuya, Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike na Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile na Wajumbe wa Mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda wakipiga picha ya pamoja na watoto waliopo kata hiyo baada ya kukabidhi jezi katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na Taasisi hiyo lililofanyika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

HABARI KATIKA PICHA