Wednesday, June 7, 2023

WANACHAMA WA OMTO WANUFAIKA NA IMBEJU YA CRDB

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule ( katikati ), Diwani wa Kata ya Kitunda, Victor Vedasto ( kushoto ), Meneja wa CRDB Tawi la Ubungo, Hollo Buyamba ( wa pili kushoto) na Meneja Mradi wa CRDB Foundation, Baraka Kiyolo ( kulia) wakiserebuka wakati wa kongamano la wajasiriamali lililowezesha kupata mitaji wezeshi kwa ajili ya kinamama wajasiriamali kupitia programu ya Imbeju lililofanyika jijini Dar es Salaam leo.


Meneja wa CRDB Tawi la Ubungo, Hollo Buyamba  akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) ikishirikiana na benki hiyo kumwezesha mjasiriamali kupata mtaji  kupitia programu yake ya IMBEJU. 

Diwani wa Kata ya Kitunda, Victor Vedasto akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) ikishirikiana na Benki ya CRDB kumwezesha mjasiriamali kupata mtaji  kupitia programu yake ya IMBEJU.

Meneja Mradi wa CRDB Foundation, Baraka Kiyolo akitoa elimu ya programu ya IMBEJU inavyomwezesha majsiriamali kupata mtaji wa biashara kupitia Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) wakati wa kongamano la wajasiriamali lililoandaliwa na Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam leo.

 Kikundi cha Kipaji Changu kikitumbuiza wakati wa kongamano hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule  ( kulia), Meneja wa CRDB Tawi la Ubungo, Hollo Buyamba ( wa pili kulia), Meneja Mradi wa CRDB Foundation, Baraka Kiyolo ( wa pili kushoto) na Diwani wa Kata ya Kitunda, Victor Vedasto wakiagana baada ya kumaliza kongamano.

Baadhi ya akina mama wajasiriamali wakihdhuria katika kongamano hilo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa benki ya CRDB, Kata ya Kitunda na Wakurugenzi wa taasisi mbalimbali katika makao makuu ya Taasisi hiyo yaliyopo Kitunda kabla ya kuelekea katika kongamano hilo.