Wazee na vijana wa mtaa wa Buguruni kwa mkanda wameanzisha utaratibu wa kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ambapo dua hii rasmi walianzisha mwaka 2020 na hivyo wanaliendeleza hili kila mwaka.
Kupitia dua hii walianzisha kikundi kiitwacho Mkanda Mshikamano chenye madhumuni ya kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa wao, kata na Taifa kwa ujumla na mwamko wa kujiunga na kikundi hicho yamekuwa ni makubwa sana. Kikundi hicho kimedhamiria kuanzisha miradi ambayo itasaidia kikundi hicho ili kuwasaidia wanachama kwa namna moja ama nyingine.
Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Mkanda Mshikamano Said Dallah alisema " Imekuwa ni mila na desturi kwa wakazi wa mkanda kufanya dua ya kuwarehemu wazee wetu kwani bila wao tusingekuwepo sisi hivyo jambo lililobakia la kumfanyia marehemu ni kumtolea sadaka na kumuombea dua kwahiyo natoa wito kwa wakazi wa mitaa mingine kuiga hili suala ".
Nae Diwani wa kata ya Mnyamani, Shukuru Dege alisema '' limekuwa ni jambo zuri sana kwa kubadilisha taswira ya makempu ya kucheza mziki tu lakini wao wanafanya majambo ya kumfurahisha mungu na kama tutaendelea hivi ninahakika kabisa dini yetu ya kiislamu itafika mbali sana".
Kutokana na upya wa Umoja huo wamekuwa na changamoto za mitaji ya kuanzisha miradi, Kibali cha kusimamia mfereji wa mtaa kwa ajili ya kuufanyia usafi, kupata makao makuu ya Kikundi.
katika hafla hiyo Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji ambaye ni mgeni rasmi alihamasisha maeneo mengine ambayo hayana utamaduni huu na pamoja na kutatua changamoto ya Ofisi ya Kikundi hicho akishirikiana na Diwani, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Ramadhani Ponela pamoja na wadau wengine walioalikwa katika dua hiyo.
Nguvu kubwa ya kuifanikisha dua hii inatokana na michango ya umoja huo ni michango ya wazawa, wakazi na viongozi wao wa serikali ya mtaa na wadau mbalimbali walioguswa na jambo hili hata kama wanaishi nje ya mtaa hivyo si tu wakazi wa hapo bali hata wa nje hili ni jambo lao na kuthibitisha hilo kuna majina ya ndugu zao wengine kutoka mitaa ya nje ya Buguruni kwa Mkanda. Hivyo wanawashukuru wote kwa kufanikisha dua yao na mungu awabariki.
Diwani wa kata ya Mnyamani, Shukuru Dege, akizungumza na wakazi pamoja na wanachama wa kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji, akizungumza na wakazi pamoja na wanachama wa kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.Ni mwaka wa pili mfululizo kwa Kikundi hicho kuwakumbuka wazee wao waliotangulia kwa kufanya tukio hilo takatifu.
Baadhi ya Masheikh wakisoma dua wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.