Mkurugenzi
wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha akizungumza na wanawake wa Kata ya Kitunda
jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake
kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto
waliokusudiwa na jukwaa hilo. Jukwaa hilo lilikuwepo hapo awali ila limefanyiwa
uhuishwaji na wanawake wa kata hiyo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wanawake Kitunda, Anna Haule (kulia) akizungumza wakati wa
uzinduzi wa jukwaa hilo la kuwezesha wanawake kiuchumi ulifanyika jijini Dar es
Salaam jana. Moja ya Lengo la Jukwaa hilo ni kuwa na sauti ya pamoja,
kutafakari na kuibua miradi mbalimbali. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa
Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha, Diwani Viti Maalum, Eva Nyamoyo na
Mwenyekiti wa UWT, Mwanaidi Makongo.]
Mkurugenzi
wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha akikata keki kuashiria uzinduzi wa jukwaa
la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto
waliokusudiwa na jukwaa hilo.
Diwani
Viti Maalum, Bi. Eva Nyamoyo akitoa somo la malezi ya watoto wakati wa uzinduzi
wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto
waliokusudiwa na jukwaa hilo. Jukwaa hilo lilikuwepo hapo awali ila limefanyiwa
uhuishwaji na wanawake wa kata hiyo.
Baadhi ya
wanawake wa Kitunda wakihudhuria katika uzinduzi wa jukwaa hilo jijini jana.
Bibi Maendeleo Kata ya Kitunda, Betty Mzava akizungumza katika hafla hiyo.
Mtendaji Kata ya Kitunda, leticia Chipando, akitoa somo la usafi mahala
pa kazi jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha
wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto
waliokusudiwa na jukwaa hilo.
Mkurugenzi
wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Viongozi mbalimbali wa Kitunda wakati baada ya kuzindua jukwaa hilo jijini
Dar es Saaam jana.