Saturday, November 25, 2023

JUKWAA LA WANAWAKE LALETA NEEMA KITUNDA

Mkurugenzi wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha akizungumza na wanawake wa Kata ya Kitunda jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa  malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto waliokusudiwa na jukwaa hilo. Jukwaa hilo lilikuwepo hapo awali ila limefanyiwa uhuishwaji na wanawake wa kata hiyo.


Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Kitunda, Anna Haule (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo la kuwezesha wanawake kiuchumi ulifanyika jijini Dar es Salaam jana. Moja ya Lengo la Jukwaa hilo ni kuwa na sauti ya pamoja, kutafakari na kuibua miradi mbalimbali. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha, Diwani Viti Maalum, Eva Nyamoyo na Mwenyekiti wa UWT, Mwanaidi Makongo.]


Mkurugenzi wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha akikata keki kuashiria uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa  malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto waliokusudiwa na jukwaa hilo.


Diwani Viti Maalum, Bi. Eva Nyamoyo akitoa somo la malezi ya watoto wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa  malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto waliokusudiwa na jukwaa hilo. Jukwaa hilo lilikuwepo hapo awali ila limefanyiwa uhuishwaji na wanawake wa kata hiyo.


Baadhi ya wanawake wa Kitunda wakihudhuria katika uzinduzi wa jukwaa hilo jijini jana.



Bibi Maendeleo Kata ya Kitunda, Betty Mzava akizungumza katika hafla hiyo.



Mtendaji Kata ya Kitunda, leticia Chipando, akitoa somo la usafi mahala pa kazi jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi pamoja na kuzindua mfuko wa  malengo ya kuwa na kituo cha kulelea watoto waliokusudiwa na jukwaa hilo.

Mkurugenzi wa Merrymerry.tz, Mery Samson Chacha ( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kitunda wakati baada ya kuzindua jukwaa hilo jijini Dar es Saaam jana.





                             

No comments:

Post a Comment