Saturday, November 18, 2023

WATEULE VICOBA WAKUTANA NA NEEMA YA OMTO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule akitoa elimu ya vicoba endelevu kwa wanachama wa Kikundi cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi huyo alialikwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.


Mwalimu wa Wateule Vicoba, Glory Munisi akitoa elimu kuhusu elimu ya fedha wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho kilichopo Ulongoni jijini Dar es Salaam jana. Wateule Vicoba inajumla ya vikundi 7 chini ya ,Mkurugenzi huyo.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo, Neema Mchau akizungumza wanachama wa Kikundi cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni kuhusu masuala ya kuthamini familia pamoja na kuimarisa ndoa wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana.


Baadhi ya Wanachama wa Wateule Vicoba wakisikiliza kwa makini mada zinazotolewa katika maadhimisho hayo.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (katikati), Katibu wa OMTO, Eliwaza Joseph na Mkurugenzi wa Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo, Neema Mchau wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza maadhimisho ya maika 12 ya Kikundi cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni jijini Dar es Salaam jana. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule ( wa tatu kulia waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya mtaa, walimu wa vicoba mbalimbali pamoja na wanachama wa Kikundi cha Vicoba cha Wateule kilichopo Ulongoni baada ya kumaliza hafla ya kuadhimisha miaka 12 ya kikundi hicho jijini Dar es Salaam jana. Mkurugenzi aliahidi kufanya mipango ya kuvisajili vikundi vyote 7 vilivyopo katika kikba hicho pamoja na kushirikiano nao ili kupata fursa zilizopo kwenye Vicoba endelevu kama CRDB Imbeju.

No comments:

Post a Comment