Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet Samson Mwazembe akizungumza na wazazi pamoja na watoto wa kata ya Kitunda katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo katika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo. Taasisi hiyo yenye kauli mbiu ya '' Malezi ya watoto na michezo vinaanzia katika jamii '' imetoa jezi za michezo katika mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda ikiwa ni miongoni mwa kusapoti sekta ya michezo nchini.
Saturday, May 22, 2021
WATOTO WA KITUNDA WAFAIDIKA NA TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION
Monday, August 24, 2020
MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA KUPATA UDHAMINI KATA YA MZINGA
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akizungumza na wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (kulia) na Mgombea Udiwani kata ya Mzinga, Job Isaack wakisalimiana na baadhi wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (katikati) na akisalimiana na mmoja wa wazee wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Nyaikoba Ryoba.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (aliyevaa shati la kijani) na Mgombea Udiwani kata ya Mzinga, Job Isaack wakila chakula katika Mgahawa unaomilikiwa na Wajasiriamali wa kata ya Mzinga baada ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam leo kupata udhamini wa fomu ya Ubunge kwa wakazi waliojiandikisha kupiga kura.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akizungumza na akina Mama wajasiriamali wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Nyaikoba Ryoba (wa pili kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Magole, Abduly Shabani Machungi ( wa tatu kushoto) akitoa shukrani kwa wakazi wa kata ya Mzinga kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa ( aliyevaa shati la kijani).