Sunday, August 8, 2021

KIKUNDI CHA MKANDA MSHIKAMANO WAFANYA DUA KUBWA YA KUWAREHEMU WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI

 Wazee na vijana wa mtaa wa Buguruni kwa mkanda wameanzisha utaratibu wa kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ambapo dua hii rasmi walianzisha mwaka 2020 na hivyo wanaliendeleza hili kila mwaka.

Kupitia dua hii walianzisha kikundi kiitwacho Mkanda Mshikamano chenye madhumuni ya kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa wao, kata na Taifa kwa ujumla na mwamko wa kujiunga na kikundi hicho yamekuwa ni makubwa sana. Kikundi hicho kimedhamiria kuanzisha miradi ambayo itasaidia kikundi hicho ili  kuwasaidia wanachama kwa namna moja ama nyingine.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Mkanda Mshikamano Said Dallah alisema " Imekuwa ni mila na desturi kwa wakazi wa mkanda kufanya dua ya kuwarehemu wazee wetu kwani bila wao tusingekuwepo sisi hivyo jambo lililobakia la kumfanyia marehemu ni kumtolea sadaka na kumuombea dua kwahiyo natoa wito kwa wakazi wa mitaa mingine kuiga hili suala ".

Nae Diwani wa kata ya Mnyamani, Shukuru Dege alisema '' limekuwa ni jambo zuri sana kwa kubadilisha taswira ya makempu ya kucheza mziki tu lakini wao wanafanya majambo ya kumfurahisha mungu na kama tutaendelea hivi ninahakika kabisa dini yetu ya kiislamu itafika mbali sana".

Kutokana na upya wa Umoja huo wamekuwa na changamoto za mitaji ya kuanzisha miradi, Kibali cha kusimamia mfereji wa mtaa kwa ajili ya kuufanyia usafi, kupata makao makuu ya Kikundi.

katika hafla hiyo Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji ambaye ni mgeni rasmi alihamasisha maeneo mengine ambayo hayana utamaduni huu na pamoja na kutatua changamoto ya Ofisi ya Kikundi hicho akishirikiana na Diwani, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Ramadhani Ponela pamoja na wadau wengine walioalikwa katika dua hiyo.

Nguvu kubwa ya kuifanikisha dua hii inatokana na michango ya umoja huo ni michango ya wazawa, wakazi na viongozi wao wa serikali ya mtaa na wadau mbalimbali walioguswa na jambo hili hata kama wanaishi nje ya mtaa hivyo si tu wakazi wa hapo bali hata wa nje hili ni jambo lao na kuthibitisha hilo kuna majina ya ndugu zao wengine kutoka mitaa ya nje ya Buguruni kwa Mkanda. Hivyo wanawashukuru wote kwa kufanikisha dua yao na mungu awabariki.


Diwani wa kata ya Mnyamani, Shukuru Dege, akizungumza na wakazi pamoja na wanachama wa kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.


Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Saady Khimji, akizungumza na wakazi pamoja na wanachama wa kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.Ni mwaka wa pili mfululizo kwa Kikundi hicho kuwakumbuka wazee wao waliotangulia kwa kufanya tukio hilo takatifu.


Katibu wa kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano, Sheikh Swaleh Asemeki akizungumza katika hafla hiyo.

Sheikh wa Wilaya ya Ilala, Sheikh Salim Mwinyipingu akipokea risala ya kikundi cha kusaidiana na kupeana fursa mbalimbali za manufaa ya mtaa cha Mkanda Mshikamano wakati hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya Masheikh wakisoma dua wakati wa hafla ya kuwaombea dua marehemu waliotangulia mbele ya haki na kuwakumbuka kwa namna nzuri ili Mungu awapunguzie adhabu za kaburi ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Ramadhani Ponela akizungumza jambo katika hafla hiyo.

                                                 HABARI KATIKA PICHA











 

Saturday, May 22, 2021

WATOTO WA KITUNDA WAFAIDIKA NA TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION

 Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe akizungumza na wazazi pamoja na watoto wa kata ya Kitunda katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo katika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo. Taasisi hiyo yenye kauli mbiu ya '' Malezi ya watoto na michezo vinaanzia katika jamii '' imetoa jezi za michezo katika mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda ikiwa ni miongoni mwa kusapoti sekta ya michezo nchini.   








Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe (Kushoto), Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Lutgarda Mbuya, Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike na Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile wakikabidhi jezi kwa mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo lililofanyika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike akizungumza katika hafla hiyo.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Lutgarda Mbuya akizungumza na wazazi na watoto wa kata ya Kitunda wakati wa Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na taasisi hiyo katika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Sauti ya Jamii wa kata ya Kitunda, Claudia Gabriel, akizungumza katika hafla hiyo.

Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile akizungumza na wazazi pamoja na watoto wa kata ya Kitunda jijini Dar es Salaam leo katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids  and Youth Foundation.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya kutoa Elimu kwa vijana na watoto kutambua vipaji vyao ya Green Kids and Youth Foundation, Vailet  Samson Mwazembe, Katibu Mtendaji wa Taasisi hiyo, Lutgarda Mbuya, Afisa Ustawi wa Jamii Kitunda, Annatholia Wabike na Mratibu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria Paralegal, Salum Kindokomile na Wajumbe wa Mashina 8 yaliyopo kata ya Kitunda wakipiga picha ya pamoja na watoto waliopo kata hiyo baada ya kukabidhi jezi katika Tamasha la Kutoa elimu ya kujitambua pamoja na unyanyasaji wa kijinsia lililoandaliwa na Taasisi hiyo lililofanyika uwanja wa Kitunda Kerezange jijini Dar es Salaam leo.

HABARI KATIKA PICHA















 

Monday, August 24, 2020

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA KUPATA UDHAMINI KATA YA MZINGA

 

Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akizungumza na wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (kulia) na Mgombea Udiwani kata ya Mzinga, Job Isaack wakisalimiana na  baadhi wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (katikati) na akisalimiana na mmoja wa wazee wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Nyaikoba Ryoba.


Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (aliyevaa shati la kijani) na Mgombea Udiwani kata ya Mzinga, Job Isaack wakila chakula katika Mgahawa unaomilikiwa na Wajasiriamali wa kata ya Mzinga baada ya kuwasili katika kata hiyo jijini Dar es Salaam leo kupata udhamini wa fomu ya Ubunge kwa wakazi waliojiandikisha kupiga kura.


Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akizungumza na akina Mama wajasiriamali wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo wakati akienda kupata udhamini kwa wakazi wa kata hiyo waliojiandikisha kupiga kura baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga, Nyaikoba Ryoba (wa pili kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa wakazi wa kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam leo.


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Magole, Abduly Shabani Machungi ( wa tatu kushoto) akitoa shukrani kwa wakazi wa kata ya Mzinga kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa ( aliyevaa shati la kijani).

HABARI KATIKA PICHA