Friday, March 6, 2020

UMOJA WA WANAWAKE KITUNDA WAFANYA ZIARA KUTEMBELEA WENYE UHITAJI MAALUM

Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka ( wa pili kushoto ), Mkurugenzi wa Taasis ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization ( OMTO ), Anna Haule pamoja na Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda msaada wa taulo za wasichana kwa wasichana waliopo katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakitoa msaada wa godoro, unga na sukari kwa Mmoja wa wakazi wa kata hiyo mwenye mazingira magumu kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika tarehe 8 machi. Umoja huo umefanya hafla ya kuwatembelea watu wenye uhitaji mbalimbali pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima cha Camp Caleb kilichopo mtaa wa Kipera kata ya Kitunda.  Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaan jana.


Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiongozana kwa pamoja wakiwa na misada yao kueleka kwa watu wenye uhitaji katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Ni miongoni wa mwa mila na desturi za umoja huo kusaidia wenye uhitaji maalum. Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaan jana.

Baadhi ya Wanawake wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakisalimiana na Mmoja wa wakazi wa Kitunda, Bibi Tausi Ramadhani baada ya kuwasili mahali alipohifadhiwa kwaajili ya kumkabidhi msaada katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. 

Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wao kwa Bibi Tausi Ramadhani katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.


Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wao kwa Mwakilishi wa Bibi anayeishi katika mazingira Magumu Bibi Salum  katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

 Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda akizungumza jambo na watoto yatima pamoja na wanaishi katika mazingira magumu baada ya kuwasili katika kituo cha Kulea watoto hao cha Camp Caleb kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili ya kutoa msaada katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiimba nyimbo za kukataa unyanyasaji wa kijinsia baada ya kuwasili katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili ya kukabidhi msaada katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

 Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka akigawa biskuti kwa  watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

 Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka ( wa pili kushoto ), Mkurugenzi wa Taasis ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization ( OMTO ), pamoja na Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda msaada wa chandarua kwa watoto waliopo katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

HABARI KATIKA PICHA














Saturday, November 23, 2019

TAASISI YA UWEZESHAJI WAJASIAMALI YA OPEN MIND AND THOUGHTS ORGANIZATION (OMTO) YALETA NEEMA KWA WATANZANIA

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia), Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakionyesha kwa pamoja Mkoba wa nyaraka za Taasisi ya OMTO katika uzinduzi wa taasisi hiyo . yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kulia) akizungumza na wajasiriamali pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana. Wapili kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola.

Mwakilishi wa Ofisi ya serikali ya mtaa ya Kitunda, Mwanahawa Zinga akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) iliyochini ya Vicoba endelevu uliofanyika ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.  Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin na Raisi wa Vicoba Endelevu, Devotha Likokola.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola akizungumza na wajasiriamali pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana. Vicoba Endelevu ni mwamvuli wa taasisi ya OMTO.



Baadhi ya Wanachama wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) pamoja na vikundi vingine vilivyopo chini ya Vicoba endelevu wakisikiliza kwa makini mada zinazoendelea wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.







       Baadhi ya wageni Waalikwa wakizungumza katika hafla hiyo.



Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (wa pili kushoto) akiitambulisha Kamati ya maandalizi ya Uzinduzi wa Taasisi hiyo uliofanyika ofisini mwa taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto), Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule, Mkurugenzi wa taasisi ya Data Sustainable Development Organization (Data), Sihaba Madenge na Mkurugenzi wa Taasisi ya Women Movement and Effort Organization (Wmeo), Anna Basita wakitumbuiza wakati wa hafla  ya uzinduzi wa taasisi OMTO yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya watoto wa wanachama wa OMTO wakitumbuiza wakati wa Uzinduzi wa taasisi hiyo.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kulia) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Taasisis ya OMTO uliofanyika ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam jana.

Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola (kushoto) akimlisha keki Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule (kushoto) akikabidhi keki kuashiria shukrani kwa Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin katika hafla hiyo. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola.

Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akikata utepe katika uzinduzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) hiyo yenye lengo la kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiriamali. Uzinduzi huo ulifanyika Ofisini mwa Taasisi hiyo Kitunda jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Raisi wa Vicoba Endelevu, Mh. Devotha Likokola na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Haule.

Mgeni rasmi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin akizungumza katika hafla hiyo.


Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) imesajiliwa rasmi tarehe 5/8/2019 ikiwa na ruhusa ya kufanya kazi ndani ya Tanzania na bara kwa kuzingatia lengo kuu la serikali la kuboresha maisha kwa kila mtanzania.

Taasisi hii imeona umuhimu wa kusaidiana na serikali na kuhakikisha lengo kuu la serikali kuwa na Tanzania ya viwanda linatimia.

Akizungumza Mkurugenzi wa OMTO, Anna Haule " Taasisi hii ina malengo yafuatayo kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za kijamii, kushawishi jamii kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali, kuhasisha jamii kuwa na tabia ya kuweka akiba ili kukuza mitaji na kufanya biashara endelevu pamoja na kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu kupitia ujasiamali". Alisema Mkurugenzi.

Taasisi kwa sasa inavikundi 15 kwa hapa Dar es Salaam na mikoni yenye jumla ya wanachama 600 ikiwemo wanawake ni 85% na wanaume ni 15%.

Kwa elimu wanayoipata ya kuweka akiba na kufanya ujasiamali wa pamoja baadhi ya vikundi tayari wameshaanza kufanya ujasiriamalikwa utengenezaji wa batiki, sabuni za maji na pilipili ya embe malengo ni kuanzisha kilimo (green house), ufugaji wa kuku, samaki na nyuki.

Nae Raisi wa Vicoba Endelevu, Mhe. Devotha Likokola akizungumza "Miongoni mwa fursa zilizopo ni kuwa pamoja katika kufanya ujasiamali ili kuwekeza kutimiza malengo ya nchi yetu ya Tanzania ya viwanda na imani kubwa ni kufikia kuwa na viwanda vidogo vidogo na kwa baadae kuwa na viwanda vikubwa". Alisema Raisi.

                  HABARI PICHA KATIKA MATUKIO




















Friday, May 11, 2018

WAKAZI WA JIMBO LA UKONGA WANUFAIKA NA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO


Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (wapili kushoto) akizungumza na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na wakazi wa mtaa huo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Vijana wajasiriamali waosha magari wa Kikundi cha  Msingi Mikwanja Car Wash yenye thamani ya shilingi milioni 1 iliyotoka katika fedha ya mfuko wa jimbo la Ukonga.Ni mwendelezo wa kutimiza ahadi ambazo Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara aliziahidi kwa wakazi wa jimbo hilo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),John Mrema.

Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto) akizungumza jambo na wakazi wa Mtaa wa Guruka Kwalala uliopo katika kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili katika mtaa huo leo kwa ajili ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash ikiwa ni mwendelezo wa kutimiza ahadi za Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala, Dorcas Rukiko,Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto,Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kushoto),Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala,   Dorcas Rukiko, Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jacob Ayo wakikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari wa kikundi cha Msingi Mkwanja Car Wash, Ally Mfaume (Wapili kulia) na Katibu Wake,Yasini Omary jijini Dar es Salaam leo.Uongozi wa Kata na mtaa pamoja Viongozi kutoka Chadema wamekabidhi mashine mbili za kuosha magari kwa Vikundi  vya Vijana wajasiamali waosha magari wa Mtaa wa Guruka Kwalala.

Diwani viti maalum pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Guruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto, Dorcas Rukiko (kushoto) akizungumza jijini Dar es Slaam leo na Vijana wa Kikundi kingine cha Vijana wajasiriamali kitwaacho Nyamachoma kinachofanya kazi ya kuosha magari maeneo ya Gongo la  mboto Mwisho wa lami katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni 1 iliyotoka katika fedha ya Mfuko wa jimbo la Ukonga ikiwa  ni Mwendelezo wa kutimiza ahadi alizoahidi Mbunge wa Jimbo hilo,Mwita Waitara.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Nyamachoma Car Wash,Juma Sungamizi,Katibu wa kikundi,Jimmy Vitalis na Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema.

    Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto, Jacob Kisi(watatu kushoto) akizungumza katika hafla hiyo.

Mashine ya Kuosha magari iliyokabidhiwa leo kwa Kikundi cha Nyamachoma Car wash kilichopo Gongo la Mboto mwisho wa lami jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akizungumza jijini Dar es Salaam leo na Vijana wajasiriamali wa Kikundi cha Kuosha magari kiitwacho Nyamachoma Car Wash katika hafla ya kukabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa kikundi hicho yenye thamani ya shilingi Milioni 1 kutoka katika Mfuko wa Jimbo la Ukonga.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akikabidhi mashine ya kuosha magari na pikipiki kwa Katibu wa Kikundi cha Vijana wajasiriamali waosha magari kiiitwacho Nyamachoma Car Wash,Jimmy Vitalis (wapili kulia) na Mwenyekiti wa kikundi hicho,Juma Sungamizi jijini Dar es Salaam leo.

Mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga pia ni Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano wa mambo ya nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mrema (kulia) akipeana mikono ya pongezi na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo baada ya kukabidhi mashine mbili za kuosha magari na pikipiki kwa Vikundi viwili vya waosha magari Nyamachoma Car Wash na Msingi Mkwanja Car Wash vilivyopo katika Mtaa wa Gruruka Kwalala kata ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam leo.