Saturday, March 4, 2023
WAKAZI WA TABATA WAKUTANA NA NEEMA YA TUWODO
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tuinuke Women Development Organization ( TUWODO ), Bi. Awena Omar Shaib akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Taasisi hiyo ipo na lengo la kuwainua kiuchumi wanawake, vijana, watoto na makundi maaalum.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Grace Mwingira akizungumza na wakazi wa Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Vilevile alitembela makao makuu ya taasisi yaliyopo Tabata Liwiti.
Baadhi ya wageni waalikwa wakisaini katika kitabu cha mahudhurio baada ya kuwasili katika ofisi ya Taasisi ya Tuinuke Women Development Organization ( TUWODO ) katika hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanachama wa Taasisi ya Tuinuke Women Development Organization ( TUWODO ) pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini elimu inayotolewa na baadhi ya wasemaji wakati wa wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika makao makuu ya taasisi hiyo Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya watoa mada wakitoa elimu ya ujasiriamali kwa wakazi wa Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tuinuke Women Development Organization ( TUWODO ), Bi. Awena Omar Shaib ( katikati) akipiga picha na wanachama wa taasisi hiyo pamoja na wageni waalikwa baada ya kumaliza kutembelea ofisi ya taasisi hiyo Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment